Maandalizi ya Kutimiza Mahitaji ya Wengine

Maandalizi ya Kutimiza Mahitaji ya Wengine

Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu. 2 WAKORINTHO 9:10

Mungu hutubariki ili tuwabariki wenzetu. Anataka mahitaji yetu yatimizwe, na anataka tujiandae kusaidia watu ambao wana mahitaji. Hii ndiyo sababu moja ambayo Mungu anaahidi kutukimu na kufanya hivyo kwa wingi.

Ili kusaidia watu wengine, tunahitaji nguvu, afya njema, na akili razini. Tunahitaji pesa kusaidia watu wanaong’ang’ana kifedha. Tunahitaji mavazi ili tuweze kuwapa watu wanaozihitaji. Tunahitaji furaha ili kusaidia wasiokuwa na tumaini.

Mungu hutupatia vitu hivyo kila wakati—na hata zaidi—kama mbegu kwa mtu ambaye anahiari kupanda (tazama 2 Wakorintho 9:9–10). Hii ina maana kuwa ukiwa mwenye shukrani kwa kile ulicho nacho, na uhiari kuwapa wengine pia, Mungu hatatimiza tu mahitaji yako, atakupa pia vitu kwa wingi ili uwe unaweza kuwapa watu wengine kila wakati. Sisi wote tunaweza kushinda vita dhidi ya uchoyo kwa kuzoea kuwa wakarimu.


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwamba unanibariki ili nibariki wengine. Nisaidie kuona mahitaji yaliyo karibu nami, na unisaidie kutekeleza jukumu langu la kutimiza mahitaji hayo. Asante kwa kuwa kumekuwa na watu ambao wamenisaidia njiani. Kwa usaidizi wako ninataka kuwafanyia wengine hivyo hivyo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon