Maisha Chini ya Agano Jipya

Maisha Chini ya Agano Jipya

Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora. — WAEBRANIA 8:6

Agano la Kale lilikuwa agano la matendo, linalotegemea sisi kutenda kila kitu wenyewe—kung’ang’ana, kupambana na kufanya kazi kwa bidii ili tukubalike na Mungu. Linatuacha tukiwa katika mtego wa kazi za mwili. Agano kama hilo linaiba furaha yetu na kututenga na Mungu.

Lakini Agano Jipya ni agano la neema, ambalo halitegemei tunaloweza kufanya, lakini kile Yesu ametufanyia tayari. Kwa hivyo, tumehesabiwa haki kwa imani sio kwa matendo ya sheria. Hizo ni habari njema sana kwa sababu tunaondolewa mshinikizo wa kutenda. Tunaweza kuacha mfadhaiko na kung’ang’ana, na kumruhusu Mungu kutenda kazi kupitia ndani yetu kwa nguvu za Roho Mtakatifu wake aliye ndani yetu.

Jambo la muhimu ni hili: Agano la Kale hutuletea utumwa; Agano Jipya hutuletea uhuru. Ndiyo kwa sababu uhusiano na Mungu, uliowezeshwa na kazi ya Yesu Kristo, ni bora kuliko kitu kingine chochote ambacho huenda tukashuhudia. Hutuweka huru kuwa tulichoumbwa kuwa halafu kufanya kile tunachopaswa kumfanyia Mungu.


Maisha katika Agano Jipya ni safari nzuri ya kuishi katika uwepo wa Mungu na kufurahia ushindi kupitia kwa Kristo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon