Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. —WARUMI 14:17
Ufalme wa Mungu una vitu ambavyo ni bora sana na vyenye manufaa kuliko mali ya dunia. Mungu hutubariki na vitu, lakini ufalme ni zaidi ya hayo: Ni haki, amani na furaha ndani ya Roho Mtakatifu.
Haki si matokeo ya mambo tunayofanya, bali ni matokeo ambayo Yesu amefanya (1Wakorintho 1:30). Yeye huchukua dhambi zetu na kisha kutupa Haki yake (2 Wakorintho 5:21). Tunapokubali huu ukweli kwa imani na kuupokea binafsi, tunakuwa huru kuishi na kufurahia maisha ambayo Yesu alikufa kutupatia.
Amani ni ya ajabu sana— bila shaka ni maisha ya ufalme. Hii ndiyo kwa sababu tunafuta amani, kuwa na hamu nayo, na kuifuatilia (Zaburi 34:14; 1 Petero 3:11). Vile tunavyomkaribia Mungu, ndivyo tunavyoelewa kwamba Yesu ni amani yetu (Waefeso 2:14). Mapenzi ya Mungu juu yangu na wewe ni, tufurahie amani yake ipitayo akili zote (Wafilipi 4:7).
Furaha inaweza kuwa kitu chochote kuanzia kwa furaha tulivu hadi kwa furaha kuu. Furaha huboresha nyuso zetu, afya yetu, na ubora wa maisha yetu. Inaimarisha ushuhuda wetu mbele ya watu na kutupatia mtazamo wa kiungu kuhusu maisha (Nehemia 8:10).
Ni wazi katika Neno la Mungu: Tafuta Mungu na Ufalme wake, na atashughulikia mengine yote (Mathayo 6:33).
Hakuna maisha mazuri kama maisha katika ufalme wa Mungu.