Mambo yote Hufanya Kazi Pamoja kwa Ajili ya Wema

Mambo yote Hufanya Kazi Pamoja kwa Ajili ya Wema

Nasi twajua na kuhakikishiwa ya kuwa [Mungu akiwa mshirika katika kazi] katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja [kutoshea katika mpango] na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kulingana na mpango na kusudi lake. —WARUMI 8:28

Mtume Paulo hasemi kwamba mambo yote ni mazuri, lakini anasema kwamba, mambo yote hufanya kazi pamoja kwa ajili ya wema.

Hebu tuseme umeingia katika gari lako, na likakataa kuanza. Kuna njia mbili ambazo unaweza kuitazama hali hii. Unaweza kusema, “Nilijua tu! huwa linatatizika. Mipango yangu huharibika kila wakati.” Ama unaweza kusema, “Ndiyo, inaonekana kwamba siwezi kuondoka sasa hivi. Nitaenda baadaye gari likishatengenezwa. Hata hivyo, ninaamini mabadiliko haya ya mipango yatafanya kazi pamoja kwa ajili ya wema wangu. Pengine kuna sababu inayonihitaji kuwa nyumbani leo, kwa hivyo nitafurahia wakati wangu hapa.”

Paulo pia anatueleza katika Warumi 12:16 kuwa “tujitayarishe kila mara kupatana na [watu, vitu].” Wazo hapa ni kwamba, lazima tujifunze kuwa aina ya mtu ambaye hupanga vitu na kutosikitika mpango huo ukiharibika.

Chaguo ni letu. Wakati wowote tunapokosa kupata tunayotaka, hisia zetu huinuka na kujaribu kutuingiza katika hali ya kujihurumia na kuwa na mawazo hasi. Ama tunaweza kuwa tayari kukabiliana na hali hiyo na kuendelea kufurahia kile alicho nacho Mungu kwa ajili yetu hata nini kifanyike.


Njia ya uhuru kutokana na uhasi huanza tunapokabiliana na tatizo na kuamini kwamba Mungu atalitumia kutenda wema.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon