Mamlaka Kupitia Kwa Maombi

Mamlaka Kupitia kwa Maombi

Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga (utakalotangaza kuwa halifai nan i kinyume cha sheria) duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua (utakalosema kuwa linalingana na sheria) duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. —Mathayo Mtakatifu 16:19

Kwa kuwa sisi sio tu viumbe wa kimwili bali wa kiroho pia, tunaweza kusimama katika ulimwengu wa kimwili na kuathiri ulimwengu wa kiroho. Hii ndiyo faida na manufaa yaliyo wazi. Tunaweza kwenda katika ulimwengu wa kiroho kupitia kwa maombi na kuleta shughuli zitakazosababisha mabadiliko katika hali fulani. “Mungu ni Roho…” (Yohana 4:24), na kila jibu tunalohitaji kwa kila hali liko naye.

Yesu alimwambia Petro kuwa atampa funguo za ufalme wa mbingu. Funguo zote hufungua milango, na ninaamini kwamba (angalau kiasi) funguo hizo zinaweza kuwakilisha aina tofauti za maombi. Yesu aliendelea kumfundisha Petro kuhusu uwezo wa kufunga na kufungua, ambao unafanya kazi kwa kanuni hiyo moja ya kiroho.

Uwezo wa kufunga na kufungua hufanyiwa mazoezi katika maombi. Wakati mimi na wewe tunaomba kuhusu kuwekwa huru kutokana na utumwa fulani katika maisha yetu au katika maisha ya mtu mwingine, tutakuwa tunafunga shida hiyo na kuachilia jibu. Tendo la maombi hufunga uovu na kuachilia mema.


Yesu ametupatia uwezo na mamlaka ya kutumia funguo za ufalme ili kutimiza mapenzi ya Mungu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon