Maneno ni Kichocheo cha Hisia

Maneno ni Kichocheo cha Hisia

Mtu azuiae kinywa chake na ulimi wake, atajilinda nafsi yake na taabu. ZABURI 21:23

Maneno huchochea hali nzuri ya moyo au hali mbaya ya moyo; kwa kweli huchochea nia na kuwa na athari kubwa kwa maisha yetu na mahusiano yetu. Tukizungumza vitu chanya na vizuri, basi tunajihubiria uzima. Tunaongeza hisia ya furaha. Lakini tukiongea maneno hasi, basi tunajihubiria mauti na dhiki; tunaongeza huzuni yetu na hali yetu ya moyo inarudi chini.

Lakini, shukuru kwamba tunaweza kudhibiti maneno tunayoongea na kiwango cha maisha yetu. Kwa nini kitu cha kwanza kila siku kisiwe kujisaidia? Usiamke kila asubuhi na kungoja kuona vile unavyohisi kisha umwambie kila atakayekusikiliza kuhusu hisia ulizo nazo. Ukifanya hivyo, unazipa hisia zako mamlaka juu yako. Badala yake, amka ukimsifu Mungu kwa wema wake katika maisha yako. Acha maneno ya shukrani yachochee maisha ya amani na furaha.


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwamba ninaweza kuchagua aina ya nia nitakayokuwa nayo kwa kuchagua kuongea maneno ya uzima kila siku. Haijalishi ninachohisi au kinachofanyika karibu nami, nitahimiza na kuimarisha roho yangu, sio mwili wangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon