Maombi Huzaa Uvumilivu Na Tumaini

Maombi Huzaa Uvumilivu na Tumaini

Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta subira; na kazi ya subira ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini. —Warumi 5:3–4

Ni rahisi kusema, “usiwe na wasiwasi.” Lakini kufanya hivyo kwa kweli huhitaji uzoefu wa uaminifu wa Mungu. Tunapomwamini Mungu halafu tushuhudie na tupitie uaminifu wake katika maisha yetu, tunapata uhakikisho mkuu wa kuishi bila kuwa na wasiwasi, hofu na mahangaiko.

Ndiyo maana ni muhimu kuendelea kuwa na imani na tumaini ndani ya Yesu katikati ya majaribu na mateso. Kwa usaidizi wa Mungu, tunaweza kupinga kwa uthabiti jaribio la kukata tamaa na kushindwa mambo yakielekea kuwa magumu. Mungu hutumia hizo nyakati ngumu za majaribu kujenga ndani yetu uvumilivu, subira, na tabia itakayozalisha uzoefu wa furaha tele na hakikisho la tumaini.

Kila mara kumbuka kwamba, unapokuwa vitani, unapata tajriba ya thamani itakayokufaidi katika siku zijazo. Utamwamini Mungu kwa urahisi hali ngumu zinapokuja, na utaweza kuwashuhudia wengine kuhusu wema na uaminifu wa Mungu. Iwapo upo vitani sasa hivi, unaweza kuruhusu vikushinde au vikutie nguvu! Fanya uamuzi ulio sawa na uache vikulete katika kiwango cha kina cha ukomavu wa kiroho.


Tunamtumikia Mungu wa ajabu, kwamba anaweza kugeuza mambo ambayo shetani alikusudia yatudhuru kuwa mema kwa ajili yetu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon