Maombi Yako ya Kipekee

Maombi Yako ya Kipekee

Toka mahali pake aketipo huwaangalia wote wakaao duniani. Yeye aiumbaye mioyo yao wote huzifikiri kazi zao zote. ZABURI 33:14–15

Kwa sababu Mungu ameiumba mioyo yetu binafsi, maombi yetu yanaweza kumiminika kwa njia ya kawaida kutoka kwa mioyo yetu na kulingana na vile alivyotuumba. Tunapoanzisha mitindo yetu binafsi ya mawasiliano na Mungu, tunaweza kujifunza kutoka kwa watu ambao huenda wana tajriba zaidi kutuliko, lakini tunahitaji kuwa waangalifu ili tusifanye kile wanachofanya wengine kiwe kipimo chetu. Shukuru kwamba, Yesu ni kipimo chetu, na ndiye kipimo cha pekee tunachohitaji.

Furahia muda wako na Bwana. Usijaribu kujilazimisha kufanya yale wengine wanafanya iwapo huna amani na mambo hayo katika roho yako. Hauna haja ya kushindana na wengine au kuiga mitindo yao ya maombi. Unaweza kwenda mbele za Mungu na shukrani moyoni mwako, ukijua kwamba anakusikia na kukupenda tu vile ulivyo. Unaweza kuomba kama mtu “mbunifu” ambaye amekuumba kuwa.


Sala ya Shukrani

Baba, ninakushukuru kwamba kila kitu kunihusu ni cha kipekee—hata jinsi ninavyoomba. Nisaidie kukung’uta ulinganishi na kuja tu kwako kwa ujasiri kama mwanao. Ninakupenda, Baba na ninapenda kutumia muda wangu kuwa nawe.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon