Matamanio Makuu ya Mungu

Tazama bikira atachukua mimba, naye atazaa mwana; nao watamwita jina lake Imanueli, yaani Mungu pamoja nasi (MATHAYO 1:23)

Yesu alikuja uliwenguni ili tuokolewe kutokana na dhambi zetu, tujumjue Mungu, na kufurahia mema yake yote katika maisha yetu. Anataka kuwa ushirika wa karibu sana nasi na kualikwa ndani ya kila kitu kinachotuhusu. Hii ndiyo kwa sababu mojawapo ya majina ya Mungu ni, Imanweli, kumaanisha, “Mungu nasi.” Anataka kuwa nasi, akihusika kwa undani katika maisha yetu. Anataka tujue sauti yake na kumfuata.

Mapenzi ya Mungu kwamba tusikie dhahiri kutoka kwake. Hataki tuishi katika hali ya kuchanganyikiwa na hofu. Tunafaa kuwa wenye uwezo wa kuamua, salama na huru. Anataka kila mmoja wetu akamilishe kudura yake na kutembea katika ukamilisho wa mpango wake kwetu.

Ndiyo, tunaweza kuiskia kutoka kwa Mungu kwa njia ya kibinafsi na ya undani. Undani wa uhusiano wetu wa kibinafsi na Mungu unategemea mawasiliano ya undani naye. Anazungumza nasi ili tuelekezwe, tuhuishwe, kurejeshwa na kufanywa wapya kila mara.

Hatua ya kwanza ya kumsikia yeyote, hata Mungu, ni kusikiliza. Geuza sikio lako kwake na utulie. Atazungumza nawe akuambie anakupenda. Mungu anataka kukutana na mahitaji yako na kufanya mengi zaidi ya vile unavyowaza au hata kufikiria (soma Waefeso 3:20). Hatakuacha wala kukusahau (soma Waebrania 13:5). Msikize na umfuate siku zote za maisha yako.

Wewe ni wa Mungu; wewe ni mmojawapo wa kondoo wake, na kondoo wanajua sauti ya mchungaji- sauti ya mgeni hawataifuata (soma Yohana 10:4-5). Unaweza kusikia kutoka kwa Mungu; ni mojawapo ya urithi wako kama Mkristo. Usiwahi kuamini vinginevyo!

NENO LA MUNGU KWAKO LEO!

Zawadi ya Mungu kwako ni maisha mapya yaliyojaa haki, amani, furaha, na undani naye.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon