
Mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli. Waefeso 4:22–24 Biblia
Mojawapo ya vitu vikubwa kuhusu uhusiano na Mungu ambavyo tunaweza kushukuru kwavyo ni kuwa wakati wote yeye hutupa mwanzo mpya. Neno lake linasema kuwa rehema zake ni mpya kila siku. Yesu alichagua wanafunzi waliokuwa na udhaifu na wa kufanya makosa, lakini aliendelea kufanya kazi nao na kuwasaidia kuwa kile walichoweza kuwa. Shukuru kuwa atakufanyia kitu hicho hicho ukimruhusu.
Mtume Paulo alisema kwa msisitizo kwamba ilikuwa muhimu kusahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele (tazama Wafilipi 3:13). Usiogope mambo yaliyopita; hayana nguvu juu yako isipokuwa zile unazoyapa. Shukuru kwa yote uliyojifunza awali, hata kutokana na makosa yako, na pia ushukuru kwamba leo ni mwanzo mpya na kwamba kitu kizuri kitafanyika!
Sala ya Shukrani
Ninashukuru, Baba, kwamba umenipa tumaini la mustakabali wangu. Asante kwamba kila siku ni mwanzo mpya, na sihitaji kamwe kudhibitiwa na mambo yaliyopita. Ninaweza kupokea rehema zako na kuamini kwa ajili ya vitu vizuri kila siku mpya.