Mkaribieni Mungu na atawakaribia ninyi. YAKOBO 4:8
Mara nyingi watu wengi huondoka kwa Mungu kwa sababu ya dhambi na makosa yao. Ushawahi kusikia au kusoma Neno la Mungu na kuhisi kuhumika? Neno la Mungu linakusudiwa kutuhakikishia dhambi zetu na kutushawishi kufanya vitu kwa njia ya Mungu, lakini halikusudiwi kutufanya tuhisi kuhukumika au tuhisi vibaya kujihusu.
Mungu anapofunua dhambi katika maisha yako, acha ikuvute kwake kwa usaidizi na msamaha, isiwahi kukufanya uondoke kutoka kwake. Kumbuka, Yesu hakufa kwa sababu ya watu watimilifu ambao huwa hawafanyi makosa, lakini alikufa kwa sababu ya watenda dhambi. Alilipia dhambi zetu ili tupokee msamaha na rehema halafu tujifunze kutokana na makosa yetu.
Tunaweza kuwa na shukrani kwamba Mungu Bwana hakutusongeza mbali naye kwa sababu ya makosa yetu. Badala yake, anatusongeza karibu naye na kuanza kutubadilisha vile anavyotaka tuwe. Muombe tu na uamini kwamba atafanya hivyo. Ni mwaminifu. Atamaliza kazi ambayo ameanza katika maisha yako.
Sala ya Shukrani
Ninakushukuru leo, Baba, kwamba umenisongeza kwako bila kujali dhambi na makosa yangu. Nisaidie nisisonge mbali nawe ninapofanya makosa. Badala yake, nisaidie kuchagua kuja kwako kwa imani, nikiamini kuwa unanipenda na unataka kunisaidia.