Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia dunaiani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. 2 MAMBO YA NYAKATI 16:9
Kadri unavyokua kwa kumkaribia Mungu, ndivyo inavyokuwa rahisi kufanya maamuzi yafaayo. Wafilipi 2:12 inasema utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. Hii ina maana kwamba baada ya wokovu wako unapozaliwa upya, unajenga uhusiano wako na Mungu kwa kusoma, kujifunza, kuomba na kwa ushirika na Mungu. Unamwalika katika kila eneo la maisha yako.
Mungu hataki kuishi katika kile ninachokiita “Sanduku la Jumapili asubuhi.” Anataka kushambulia kila siku ya maisha yako na kuhusika katika kila kitu unachofanya. Shukuru kwamba Mungu ni mshiriki wako katika maisha. Anafurahia kukusaidia, na haswa anafurahia tu kuwa nawe! Katika njia zako zote mkiri Mungu naye atayanyosha mapito yako (tazama Mithali 3:6).
Sala ya Shukrani
Baba, ninatamani kukupa kila eneo la maisha yangu. Ninakushukuru kwa kuwa nguvu zako ni nyingi zaidi kiasi kwamba haziwezi kufungiwa katika eneo moja tu la maisha yangu. Leo ninachagua kusalimisha kila eneo la maisha yangu na kila kitu nilicho nacho—wakati wangu, nguvu, vipawa, fedha, mahusiano na hisia—kwako.