Mkubaliwa wa Mungu

Mkubaliwa wa Mungu

Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wandamu. —LUKA 2:52

Kutoka utotoni, Yesu alitembea katika kibali cha kimiujiza cha Mungu na wanadamu. Kwa kweli punde tu alipoanza huduma yake kwa umma, alikuwa maarufu sana kiasi cha kukosa muda wa kuwa peke yake katika maombi na kuwa na ushirika na Baba yake wa mbinguni. Hata wale ambao hawakumwamini walitambua kwamba alifurahia neema ya Mungu. Mafarisayo walipowatuma watumishi kumshika Yesu, walirudi wakisema, “Hajanena kamwe mtu yeyote kama huyu anavyonena!” (Yohana 7:46). Hadi kufikia mwisho wa maisha yake, hata msalabani, hicho kibali na uwezo wa kipekee vilitambuliwa (Luka 23:47-48).

Hivyo ndivyo tunavyohitaji kujiona: kama wakubaliwa wa Bwana. Hatuoni kama viumbe dhaifu, visivyojiweza na vyenye dhambi. Hutuona tukiwa tumevishwa haki, viatu vya amani, tukiwa tumepambwa kwa silaha zote za Mungu, na tukiinua upanga wa Roho, ambalo ni Neno la Bwana (Waefeso 6:13-17). Hivyo ndivyo tunapaswa kujiona.

Watoto wetu wana kibali chetu na wakati wowote tunapoweza, tunawasaidia. Hebu fikiria tu ukweli huu ulivyo kwetu sisi kama wana wa Mungu. Haijalishi vile tunavyojiona au vile wengine wanavyotuona, hatufai kamwe kusahau kwamba Mungu anaweza kusababisha nuru ya kibali chake kung’aa juu yetu—vile tu alivyomfanyia Yesu!


Jione vile Mungu akuonavyo na upate kufurahi kuhusu urithi wako ndani yake.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon