Moyo Mtimilifu

Moyo Mtimilifu

Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama. EZEKIELI 11:19

Ingawa tabia zetu haziwi timilifu kila wakati, inawezekana kwetu sisi kuwa na moyo mtimilifu kwake Mungu. Hiyo ina maana tunampenda kwa moyo wetu wote, na tunataka kumpendeza na kufanya yaliyo mema.

Tunapompokea Yesu kama dhabihu iliyo timilifu kwa ajili ya dhambi, anatupatia moyo mpya na kuweka Roho wake ndani yetu. Moyo anaotupa ni wenye shukrani, safi, na mtimilifu kwake. Ninapenda kusema kwamba, anatupatia “ninataka ku” mpya. Anatupatia hamu ya kutaka kumpendeza.

Kwa kweli kile Mungu anataka ni sisi kumpenda, na kutokana na upendo huo, tufanye tuwezavyo kumtumikia na kumtii. Tukifanya vizuri tuwezavyo kila siku, ingawa kile kizuri tunachofanya bado kimepungukiwa, Mungu huona mioyo yetu na hata hivyo kutuona kama watu walio watimilifu kwa sababu ya neema yake (neema na baraka tusiyostahili).


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru leo, Baba, kwamba unaona nia ya moyo wangu. Ninajua kwamba umenipa “ninataka ku” mpya, na kwa usaidizi wako, nitafanya niwezavyo kukupendeza kwa matendo yangu. Ninakupenda, Baba, na ninakushukuru kwa neema yako katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon