Moyo Wa Furaha

Moyo wa Furaha

Siku zote za mtu ateswaye ni mbaya; bali ukunjufu wa moyo ni karamu ya daima. —Mithali 15:15

“Ubashiri mwovu” ni hisia isiyo dhahiri inayotisha kwamba kuna kitu kibaya kitakachofanyika. Kuna wakati ambao niligundua kuwa nilikuwa na hisia hizi kwa miaka mingi ya maisha yangu. Kwa kweli nilikuwa nimetaabishwa na mawazo maovu na ubashiri.

Pengine una hisia hizi pia. Una hali ambazo ni ngumu sana, lakini hata kama huna, bado unataabika kwa sababu fikra zako zinasumisha mwono wako na kukunyima uwezo wa kufurahia maisha na kuona siku njema.

Mithali 15:15 inakuahidi kwamba hisia hizi hazifai kudumu. Fikra za imani ni za kumwegemea Mungu, kumwamini na kumtumainia- ni jambo la furaha kusherehekea kwa matarajio ya wema. Badala ya kuogopa kitu kwa kutarajia kuwa kitakutaabisha, unaweza kuwa na imani kuwa Mungu atakupa uwezo wa kukifurahia. Furaha, amani, haki, na nguvu zako ziko ndani yako kupitia kwa uwepo wa Roho Mtakatifu. Usiache wasiwasi na fadhaa vitawale katika maisha yako. Tarajia usaidizi wa Mungu, baraka na nguvu katika kila kitu unachofanya.


Na fikra zinazofaa, unaweza kutiwa nguvu za kufanya kazi za kawaida za ulimwengu kwa furaha kuu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon