Moyo wa Tai

Moyo wa Tai

Kwa sababu hiyo nakukumbusha uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako… 2 TIMOTHEO 1:6

Ushawahi kuhisi kama tai katika kibanda cha kuku? Unajua katika moyo wako kwamba kuna mengi kuliko yale unayoyafanya na kudhihirisha katika maisha yako sasa hivi. Unahisi kwa hakika kwamba Mungu ana kusudi kubwa kwa ajili ya maisha yako—na huwezi kukwepa au kupuuza himizo la ndani la “kiendee.”

Ninakuhimiza leo kuchochea karama iliyo ndani yako. Ichochee hadi iangaze zaidi. Usiwahi kukata tamaa kwa ukuu ulioumbiwa, na usiwahi kujaribu kuficha upekee wako. Badala yake, shukuru kwao, na ushukuru kwamba Mungu ana kitu spesheli kwa ajili yako. Tambua kwamba njaa yako ya vituko ni ya kupewa na Mungu; kutaka kujaribu kitu kipya ni hamu ya ajabu; na kukumbatia maisha na kulenga juu ndiyo uliumbiwa. Wewe ni tai!


Sala ya Shukrani

Baba, asante kwa ndoto na matamanio ambayo umetia moyoni mwangu. Asante kwa kuwa una hatima kwa ajili yangu. Leo nitajaribu kuota kuhusu vitu vyote vya ajabu ulivyonavyo katika mpango wako juu ya maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon