Moyo wenye Kiburi

Moyo wenye Kiburi

. . . Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. —YAKOBO 4:6

Mungu amewahi kukabiliana nawe kuhusu kiburi? Hizi hapa baadhi ya njia unazoweza kujua iwapo una tatizo la kiburi: Iwapo una maoni kuhusu kila kitu, iwapo wewe ni wa kuhukumu, ikiwa huwezi kurekebishwa, ukiasi mamlaka, ikiwa unataka pongezi zote ziende kwako, au ukiwa unasema “mimi” kila mara. Hizi ni dalili za kiburi.

Ni vigumu kuruhusu Mungu kubadilisha kiburi chetu na unyenyekevu, lakini ni muhimu. Tukitaka kuishi katika uhusiano wa karibu na Mungu, lazima tuje kwake na fikra za unyenyekevu. Kiburi hujitegemea, lakini unyenyekevu humtegemea Mungu. Ni katika mahali tu pa unyenyekevu ambapo Mungu huweza kutubariki.

Wanyenyekevu hupata usaidizi! Jidhilini mbele za Bwana, naye atawatukuza (Yakobo 4:10). Watu wenye kiburi hufikiri wanastahili kupata kila kitu wanachotaka “saa hii,” lakini unyenyekevu unasema, “Nyakati zangu ziko mikononi mwako, Bwana.”


Kiburi husema “Ninaweza,” lakini unyenyekevu husema, “Kristo kupitia kwangu anaweza.”

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon