Mpango Mkubwa Zaidi

Mpango Mkubwa Zaidi

Yesu akawakazia macho, akawaambia, kwa wanadamu, hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana. —MATHAYO 19:26

Ni muhimu kuomba Mungu akupe ndoto na maono ya maisha yako. Tunaishi bila maono yoyote. Mungu ametuumba tuwe na malengo. Waefeso 3:20 inatuambia, basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawezayo… Hii ndiyo kwa sababu, kama Wakristo, tunaweza kuwaza mawazo makubwa, tuwe na malengo makubwa, na kutumainia vitu vikubwa.

Mara nyingi tunaangalia kazi na kufikiri hakuna vile tunaweza kufanya kinachohitajiwa kufanywa. Hili hufanyika tunapojiangalia badala ya kuangalia Mungu, ambaye anaweza kufanya mambo yote.

Mungu alipomwita Yoshua kuchukua mahala pa Musa na kuongoza wana wa Israeli hadi kwenye Nchi ya Ahadi, alimwambia, “vile nilivyokuwa na Musa, vivyo hivyo nitakuwa nawe; sitakupungukia wala sitakuacha” (Yoshua 1:5).

Mungu akiahidi kuwa nasi—na huwa anafanya hivyo—kwa kweli hilo ndilo tunahitaji. Uweza wake hutimilika katika udhaifu (2 Wakorintho 12:9). Hata kama una udhaifu gani, uweza wa Mungu upo kufanya vitu vikubwa katika maisha yako kuliko vile ulivyofikiri inawezekana.


Mungu hupata heshima unapomtumainia kufanya vitu vikubwa ambavyo kwa kweli vinaonekana kutowezekana.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon