Mpango Mzuri Wakati Wowote

Mpango Mzuri Wakati Wowote

Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. YOHANA 3:16

Nimepewa mipango inayoweza kufanywa mara moja maishani na kuyabadilisha, na nimepata kwamba sio mizuri kama vile inavyosikika. Mara nyingi huwa inakusudiwa kutugusa hisia ili tufanye uamuzi wa haraka ndipo tusikose hii “nafasi moja maishani, ambayo haiwezi kutokea tena.”

Shukuru kwamba kile Mungu anapeana ndani ya Yesu sio mzaha wa mauzo. Kinaweza kufikiwa na mtu yeyote, wakati wowote anaokihitaji! Yesu, kibadala cha upatanisho, alilipia adhabu yetu. Alikuwa mwenye hatia ili tusiwe na hatia, ilhali alichukua maovu yetu (tazama Isaya 53:11). Ishi maisha yako leo ukishukuru kuwa wokovu wako ni kipaji cha bure. Hakuna mpango ulio mkubwa kuliko huo!


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba nina hakikisho la maisha ya milele mbinguni nawe. Asante kuwa Yesu alichukua dhambi zangu na kunipa haki yake. Nitaishi kila siku nikiwa na shukrani kwa maisha yangu mapya ndani ya Yesu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon