Mtu Jasiri Huepuka Ulinganishi

Mtu Jasiri Huepuka Ulinganishi

Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure… 1 WAKORINTHO 15:10

Ujasiri hautawezekana kama bado tunajilinganisha na watu wengine. Hata kama tunaonekana vizuri, tuna vipawa au werevu, au tumefanikiwa, kuna mtu kila wakati ambaye ni bora kutuliko, na hivi karibuni tutakutana naye.

Ninaamini ujasiri hupatikana katika kujua Mungu anatupenda, kutambua vipaji tulivyo navyo na kushukuru kwa ajili ya vipaji hivyo—halafu tutie bidii tuwezavyo kufanya kazi na kile Mungu ametupatia kufanya kazi nacho. Ujasiri haupatikani katika kujilinganisha na watu wengine na kushindana nao.

Kung’ang’ana kila mara kudumisha nafasi ya kwanza ni kazi ngumu. Kwa kweli haiwezekani. Hatufai kupata furaha yetu katika kuwa bora kuliko wengine, lakini kwa kuwa bora tuwezavyo kwa ajili ya Bwana.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Baba, kwamba si lazima niwe bora kuliko wengine ndipo unikubali. Nina ujasiri na usalama kwa sababu ninajua unanipenda jinsi nilivyo. Asante kwa amani inayokuja ninapokataa kujilinganisha na wengine.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon