Mungu Ana Majibu

Bwana akujibu siku ya dhiki, jina la Mungu wa Yakobo likuinue  (ZABURI 20:1)

Iwapo ushawahi kuwa katika uhusiano, kujaribu kudhibiti pesa zako, kuwa na kazi, kujaribu kutambua na kutimiza kusudi la Bwana juu ya maisha yako, au kujaribu kukua kiroho- basi pengine umekumbana na baadhi ya matatizo. Matatizo ni sehemu ya maisha na unapomaliza tatizo moja, huenda ukawa na nyingine inayofuatia mara moja hiyo! Huo ni ukweli kwetu sisi wote na hata ingawa tunaweza kukua na kukomaa katika uwezo wetu wa kukabili, kuvumilia, kuwa wakakamavu, na kuishi katika ushindi, tutakuwa tu tukikabiliana na shida moja au nyingine.

Ni Mungu peke yake aliye na suluhu kwa shida za maisha, na kitu kizuri sana tunachoweza kufanya na shida zetu, ni kumpa. Tunahitaji kuacha kuzikariri katika akili zetu, kuacha kuzungumza kuzihusu, kuacha kuzihangaikia kuachia Mungu shinikizo na shida za maisha na kuacha abadilishe kila kitu. Tukijifunza kusalimisha mifadhaiko na hali zetu kwa Mungu, tutafurahia maisha yetu zaidi, watu watafurahia kuwa karibu yetu, na tutakuwa na furaha na utulivu zaidi.

Mungu anaweza kufanya mengi katika wakati mmoja kuliko vile tunavyoweza kufanya katika muda wote wa maisha kwa kupambana na kung’ang’ana. Anaweza kuzungumza nawe kwa sekunde tu na kugeuza hali kabisa; neno moja kutoka kwake linaweza kusuluhisha kila kitu. Hakuna kitu kikubwa kinachoweza kumshinda Mungu kutimiza, na hakuna kitu kidogo asichoweza kujali. Anajali kila kitu kinachokuhusu, kwa hivyo mpe shida zako na umwache akupe suluhu unazohitaji.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mpe Mungu shida zako na umruhusu kukupa suluhu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon