Mungu ana Mpango Mzuri wa Maisha yako

Mungu ana Mpango Mzuri wa Maisha yako

Hakika wema na fadhili zitanifuata siku zote za maisha yangu; nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. —ZABURI 23:6

Zaburi 23 ni sura yenye nguvu ya Biblia ambayo inaeleza hali ambayo Mungu anataka tuishi kila wakati. Anataka tulindwe, tuongozwe na kufarijiwa. Anataka kuandaa meza ya baraka mbele yetu machoni pa watesi wetu. Anataka anataka kutupaka mafuta ya furaha badala ya maombolezo. Anataka kikombe chetu cha baraka kifurike kila wakati katika shukrani na sifa kwake kwa sababu ya wema, fadhili na upendo usiokoma kwetu. Na anataka tuishi kila siku na kila wakati tukiwa salama katika uwepo wake.

Huku “kutaka” kote ni mojawapo ya mipango mizuri ya Mungu kwa kila mmoja wetu. Hata kama tumerudi nyuma vipi, anataka kuturejesha karibu naye na katika huo mpango mzuri na mtimilifu alio nao juu ya maisha yetu.

Itafaidi kila mmoja wetu iwapo tutajiambia mara nyingi kwa siku, “Mungu ana mpango mzuri wa maisha yangu. Ninataka yote anayonitakia. Ninapokea upendo na wema wake katika maisha yangu. Nitatembea na kuishi katika uwepo wa Bwana.”


Kumbuka kwamba kitu muhimu kabisa katika kupokea baraka za Mungu sio imani yetu kuu bali uaminifu wake mkuu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon