Mungu Anaweza Kutumia Watu Tusiotarajia Kamwe

Mungu Anaweza Kutumia Watu Tusiotarajia Kamwe

Bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu. 1 WAKORINTHO 1:27

Mara nyingi Mungu huchagua wale watahiniwa wasiotarajiwa kabisa kufanya kazi. Ana mlango mkubwa mpana wa kuonyesha vile neema na nguvu zake zinaweza kubadilisha maisha ya binadamu.

Kila mmoja wetu ana kusudi na hakuna sababu kabisa ya kutolitimiza. Hatuwezi kutumia udhaifu wetu kama sababu, Mungu anasema uweza wake hutimilika katika udhaifu (tazama 2 Wakorintho 12:9). Hatuwezi kutumia mambo ya nyuma kama sababu, kwa sababu Mungu anatuambia ya kale yamepita, yamekuwa mapya (tazama 2 Wakorintho 5:17).

Shida sio vile Mungu anavyotuona, mara nyingi ni vile tunavyojiona ndiyo hutufanya tusifanikiwe. Iwapo utajiona vile Mungu hukuona, ukiwa mwenye shukrani kwa nguvu zake za kugeuza, hakuna kizuizi kinachoweza kukomesha makusudio yake juu yako. Umeumbwa upya kwa mfano wa Mungu na kufufuliwa kwa maisha mapya kabisa. Kusudio lako linakungoja ulidai!


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru, Mungu, kwamba unachagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu. Asante kwa kuwa hakuna sababu inayoweza kunizuia kutimiza kusudi langu ndani yako. Maisha yangu ni yako, tenda kupitia kwangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon