Mungu hufanya kazi kupitia watu

Mungu hufanya kazi kupitia watu

Tena walitenda hivi si kama tulivyotumaini tu, bali kwanza walijitoa nafsi zao kwa Bwana; na kwetu pia, kwa mapenzi ya Mungu.  —2 Wakorintho 8:5

Asubuhi moja nilikuwa na wakati wangu wa utulivu peke yangu na Mungu, na nikamwambia Bwana, “Je! Unawezaje kusimama kuona watoto wako wote wanaopata maumivu, biashara haramu ya kibinadamu, mauaji ya kijumla, udhalimu, uharibifu, umasikini duniani na hufanyi kitu ? ”

Sikuwa nasema kama malalamiko au kwa sababu nilikuwa nikihoji uaminifu wake, na sijui hata kama nilikuwa nikitarajia kupata jibu, lakini nilimuuliza tu. Mara jibu lake lilirudi: “Ninafanya kazi kupitia watu. Ninasubiri watu wangu wainuke na kufanya kitu. ”

Wewe na mimi ni sehemu ya jeshi, mwili wa Kristo, na itachukua kila mtu kufanya sehemu yake ya kubadilisha dunia hii. Mungu anataka kufanya kazi kupitia kwetu, na Yeye anatuita sisi kuenenda katika upendo na kufanya kazi.

Katika 2 Wakorintho 8, Paulo alizungumza juu ya jinsi makanisa ya Makedonia yalitoa, akisema.

Tena walitenda hivi si kama tulivyotumaini tu, bali kwanza walijitoa nafsi zao kwa Bwana; na kwetu pia, kwa mapenzi ya Mungu.

Hiyo inashangaza sana, kwa sababu hawakupeana fedha zao tu – walijitoa wenyewe. Mungu anatuita sisi kuishi vivyo hivyo. Na mtu mmoja anayefanya kazi kwa Bwana ana uwezo wa kufanya tofauti kubwa! Kwa hiyo utajitoaje kwa Bwana na kuwa wakala wake leo?


Ombi La Kuanza Siku

Mungu, ninakualika kufanya kazi kupitia mimi. Ninaamua kuweka ubinafsi na kuuchukua upendo ili nipate kutumika na Wewe kubadili ulimwengu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon