Mungu hufungua na kufunga milango

Mungu hufungua na kufunga milango

Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye. Ufunuo wa Yohana 3:7 

Kuna nyakati muhimu katika maisha yetu wakati tunapohitaji hasa kujua tunasikia wazi kutoka kwa Mungu. Si rahisi sana kujua sauti Yake ikilingana na ile ya mawazo yetu ya kihisia. Lakini najua kutokana na uzoefu kwamba Mungu anaweza kufungua milango ya nafasi ambayo hakuna mtu anayeweza kuifunga, na anaweza pia kufunga milango ambayo hatuwezi kufungua.

Nilikaa miaka mingi nikijaribu kufanya mambo kutokea kama nilivyotaka katika maisha. Matokeo yake ilikuwa kuchanganyikiwa na kukatishwa tamaa. Lakini nimeona kwamba tunapomtegemea Mungu, atatupa neema na kufanya mambo kuwa rahisi kwetu tunapomtafuta Yeye na wakati wake kamili. Anatuongoza hatua moja kwa wakati. Ikiwa unachukua hatua moja mbele katika mwelekeo usio sahihi, atakujulisha kabla ya kwenda mbali sana. Kumbuka kwamba mawazo Yake yako juu ya mawazo yako. Anaona mwisho tangia mwanzo. Njia zake zote ni sahihi na hakika. Anajua kinacho na maana kwa maisha yako na anaweza kufanya hayo kutokea. Sikiliza sauti yake na hutadanganywa.

 OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, naamini kwamba utafungua milango ya haki katika maisha yangu na ufunge ile isiofaa. Hata wakati sijui cha kufanya, nina imani kwamba ninaweza kusikia kutoka kwako na kufuata mapenzi yako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon