Mungu Huwasilisha Ujumbe Wake

Basi isikize sauti ya Bwana, Mungu wako (KUMBUKUMBU LA TORATI 27:10)

Wakati mwingine Mungu huzungumza nasi kupitia kwa watu wengine, kama unavyojua. Ninakumbuka wakati fulani Mungu alipozungumza nami kupitia kwa Dave kuhusu kitu katika maisha yangu. Aliponiambia, nilikasirika. Dave alisema tu, “fanya upendavyo nalo; Ninakuambia tu ninachoamini kwamba Mungu alinionyesha.” Hakujaribu kunishawishi kwamba alichosema ni ukweli; aliripoti tu alichoamini Mungu alikuwa amemwambia. Katika muda wa siku tatu zilizofuatia, Mungu alinishawishi kwamba neno alilokuwa amempa Dave lilikuwa sahihi. Nilitiririkwa na machozi mengi kwa kuwa niliona aibu kukubali kwamba Dave alikuwa sahihi!

 

Kupitia kwa neno la maarifa ambalo Mungu alinipa kupitia kwa Dave niliweza kuelewa ni kwa nini nilikuwa na mashaka katika eneo fulani la maisha yangu. Nilikuwa nikimtafuta Mungu kuhusu hali hii na sikuwa nikipata majibu yoyote. Dave alikuwa amenipa jibu langu, lakini sikulipenda kwa sababu lilinithibitishia kwamba nilikuwa na dhambi za kuhukumu na masengenyo. Ukweli kwamba sikutaka kusikia hilo, ndiyo huenda ikawa sababu ya Mungu kumpa Dave- kwa sababu alijua nisingeisikia kutoka kwake mwenyewe.

Siwezi kusisitiza kupindukia matokeo ambayo tajriba ilileta katika maisha yangu. Kama Mungu angenishughulikia moja kwa moja, nina hakika ningejifunza funzo, lakini lisingekuwa kama funzo nililojifunza kwa sababu alizungumza nami kupitia kwa Dave.

Ninakuhimiza kujifungua kumsikia Mungu akizungumza nawe kupitia kwa watu wanaoaminika ambao husikia sauti yake na kukupenda kiasi cha kusema kile ambacho anataka usikie.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO: Mwombe Mungu kila siku azungumze nawe viwavyo, wakati wowote, na kupitia kwa yeyote anayependa.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon