Mungu ni Mwema Kila Wakati

Mungu ni Mwema Kila Wakati

Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. —YAKOBO 1:17

Yakobo anatuambia kuwa Mungu ni mwema, tosha. Si ati huwa mwema wakati mwingine; ni mwema kila wakati.

Si ni jambo la ajabu kuwa na Mungu ambaye habadiliki? Na Mungu hakuna kubadilika wala kivuli cha kugeuka-geuka. Tunaweza kumtegemea kuwa mwaminifu kila wakati, kwa mwenye huruma na kusamehe kila wakati, kututendea tu mema wakati wote wa maisha yetu.

Tunapokuwa na wakati mgumu, tukihisi kukata tamaa, bado Mungu ni mwema. Yeye si mwanzilishi wa matatizo yetu. Kitu kibaya kikifanyika kwetu, bado Mungu ni mwema. Hatufanyii mambo mazuri kwa sababu sisi ni wazuri na tunastahili; anatufanyia kwa sababu ni mwema na anatupenda. Tunaweza kutegemea wema wa Bwana katika maisha yetu!


Ufunguo wa furaha na utimilifu sio kubadilisha hali au mazingira yetu, lakini katika kumwamini Mungu kuwa Mungu katika maisha yetu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon