Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu—nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu—nimhofu nani? ZABURI 27:1
Mustakabali umeshikilia mchanganyiko wa vitu tutakavyofurahia na vitu ambavyo tunaweza kuisha bila kuwa navyo lakini vyote vitakuja. Katika Wafilipi 4:11– 12, Paulo alipitia nyakati za kudhiliwa na nyakati za kufanikiwa, lakini alisema pia kwamba aliweza kuridhika katika nyakati zote, nasi pia tuna chaguo hili (na uwezo) kama kipaji kutoka kwa Mungu. Ninashukuru Mungu sana kwa uwezo wa kuimarika kwa kuwa niliharibu wakati mwingi sana nikikasirika kuhusu vitu ambavyo nisingeweza kudhibiti.
Yesu alituahidi kuwa ulimwenguni tutakuwa na dhiki, lakini alituambia “tujipe moyo” kwa sababu aliushinda ulimwengu na kuchukua nguvu zake za kutudhuru (tazama Yohana 16:33). Fanya maisha yawe ya kufurahia kabisa; shukuru kwayo, usiyaogope. Yakabili kwa ujasiri na useme, “Sitahofu, kwa sababu aliye ndani yangu ni mkuu kuliko aliye ulimwenguni” (tazama1 Yohana 4:4).
Sala ya Shukrani
Ninakushukuru leo, Baba, kwa kuwa ninaweza kuwa na nia chanya inayotazamia makuu kuhusu mustakabali wangu kwa kuwa ninajua siko peke yangu. Haijalishi kizuizi ninachopinga ninaweza kujipa moyo kwa sababu umeushinda ulimwengu.