Mwaminifu wa Kusamehe

Mwaminifu wa Kusamehe

. . . Dhambi zao na uasi wao s itaukumbuka t ena kabisa. WAEBRANIA 10:17

Wakati wote Mungu huwa mwaminifu kutusamehe dhambi zetu vile tu alivyoahidi atafanya. Wakati mwingine watu huwa hawatusamehi, lakini wakati wote Mungu husamehe na kusahau dhambi. Na tunaweza kushukuru kujua kwamba hakuna mipaka kwa msamaha wa Mungu.

Mara nyingi watu huwa na mipaka ya vile vitu wanahiari kusamehe na mara ngapi wanahiari kusamehe, lakini msamaha wa Mungu huwa hauishi. Huenda watu wakasema wametusamehe, halafu watukumbushe kile tulichofanya ambacho kiliwaumiza, lakini Mungu huwa hatukumbushi ya nyuma, kwa sababu ameyasahau (tazama Waebrania 10:17).

Tunapokumbushwa dhambi za hapo nyuma, sio Mungu hutukumbusha; ni Shetani mshtaki wa watu wa Mungu. Kataa uongo wa adui, na uchague kupokea uaminifu wa Mungu wa kukusamehe.


Sala ya Shukrani

Ninakushukuru leo, Baba, kwamba wewe huwa mwaminifu wa kusamehe wakati wote. Hata nikikosea mara ngapi, ninajua kuwa unanipenda na wewe ni mwaminifu kusamehe dhambi zangu. Ninashukuru kwa sababu ya msamaha wako na ninataka kuishi vizuri niwezavyo kwa ajili yako kama mwitiko wa wema wako kwangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon