Mwepesi wa Kusamehe

Mwepesi wa Kusamehe

Mkichukuliana na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kulaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. WAKOLOSAI 3:13

Ulimwengu umejaa uchungu na watu wanaoteseka; na kutokana na tajriba yangu, nimetambua kwamba watu wanaoteseka hutesa wengine. Shetani hufanya kazi bila kupumzika miongoni mwa watu wa Mungu kuleta kukosana, ugomvi na migawanyiko, lakini tunaweza kushukuru kwamba Mungu anatupatia kifaa cha kumsikitisha na kumshinda shetani: Tunaweza kuwa wepesi wa kusamehe.

Msamaha hufunga mlango kwa mashambulizi ya shetani ili asipate nafasi na hatimaye kuja kuwa ngome. Unaweza kuzuia au kumaliza ugomvi katika uhusiano wetu na wengine. Si ajabu Maandiko hutuambia kila mara kwamba tunafaa kusamehe wale wanaotukosea au kututesa. Yesu alifanya msamaha kuwa mtindo wa maisha, na akatufundisha kufanya vivyo hivyo. Hili ni muhimu kwa kuishi maisha yaliyojaa furaha.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru sana kwa msamaha ulionipa kupitia kwa Yesu na kwa neema ya kuniwezesha kuwasamehe wengine. Haijalishi vile wengine walivyonikosea au kunitesa, leo ninachagua kusamehe walionisababishia uchungu. Asante kwa kunisaidia kuishi maisha ya msamaha huo kila siku mpya.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon