Mwezeshaji wa Kiungu

Mwezeshaji wa Kiungu

Tazama mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?—YEREMIA 32:27

Mungu wetu anaweza kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu (Waefeso 3:20). Tunapoomba kwa imani, inafungua mlango kwa Mungu kufanya kazi katika maisha yetu. Hakuna gumu asiloliweza.

Iwapo unang’ang’ana na mabadiliko ambayo yanahitaji kufanywa vile unavyotaka, hili ni neno lako haswa. Huwezi kujibadilisha. Lakini shukrani kwa Mungu, anaweza! Anajua kasoro zako na yuko tayari na anaweza kuleta mabadiliko unayohitaji ukimwomba tu.

Wewe na mimi hatuna shida kubwa kushinda neema ya Mungu. Shida yetu ikiwa kubwa, neema ya Mungu inakuwa kubwa zaidi. Shida zetu zikiwa nyingi, neema ya Mungu pia inakuwa nyingi pia ili tuweze kuzishughulikia.

Si vigumu Mungu kutuokoa kutoka kwa matatizo matatu kuliko vile ilivyo yeye kutuokoa kutoka kwa tatizo moja au mawili. Tatizo letu kubwa bado ni dogo kwake. Mungu anaweza kufanya kitu chochote, kwa hivyo omba kwa imani, utulie na uache afanye kazi.


Mungu alijua makosa yetu yote alipotukubali, na hatawahi kutukataa kwa sababu hiyo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon