Ndiyo Njia Bora

Lakini mimi nawaambia iliyo kweli, yawafaa ninyi mimi niondoke kwa maana mimi nisipoondoka huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu (YOHANA 16:7)

Uwepo wa Roho Mtakatifu katika maisha yetu ni wa ajabu kuliko vile tunavyoweza kufikiri. Yeye ni Mfariji wetu na hilo lina maana kwamba atatusaidia na kutufariji wakati wowote tunapodhuriwa katika safari yetu ya maisha. Ninapenda kusikia kuhusu Roho Mtakatifu kama ambaye yuko karibu nami kama pumzi yangu inayofuatia.

Roho Mtakatifu hutuongoza na kutuelekeza katika mpango wa Mungu juu ya maisha yetu. Kujifunza kufuata uongozi wake ni safari. Tumezoea kuishi kwa mawazo yetu, hisia na matamanio, laikini kama Wakristo tunahitaji kujifunza kuongozwa na Roho Mtakatifu. Yesu alikuja katika mwili wa mwanadamu na anaelewa yote tunayopitia katika maisha. Inanipa faraja kuu kukumbuka kwamba Yesu ananielewa! Ni mwenye subira na ataendelea kufanya kazi nasi bora tu tuwe tunahiari kuendelea kujifunza.

Kwa nini Yesu atasema kwamba itakuwa bora kwake kwenda na kutuma Roho Mtakatifu? Nini hicho kitakuwa bora kuliko kuwa na Yesu mwenyewe duniani? Yesu angekuwa tu mahali pamoja kwa wakati mmoja lakini Roho Mtakatifu anaweza kuwa kila mahali, akifanya kazi ndani ya kila mmoja kwa wakati mmoja. Inashangaza! Huwa hatuachi, sio hata kwa dakika moja. Anajua kila kitu kutuhusu na anafanya kazi kuponya vile vyote ambavyo vimevunjika au kuumizwa ndani yetu, na kuweka kila kitu katika utaratibu wake wa kufanya kazi. Tunakuwa bora na bora kila siku kwa njia zote kupitia kwa nguvu na hekima ya Roho Mtakatifu.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mwombe Roho Mtakatifu kukuchukua jinsi ulivyo na kukufanya anachotaka uwe.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon