Neema na Wingi wa Shukrani

Neema na Wingi wa Shukrani

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu. WAEFESO 2:8

Ni vigumu—iwapo haiwezekani—kwa kweli kuwa wenye shukrani na kushukuru hadi tuelewe neema ya Mungu. Neema ni kibali tusichostahili, lakini pia ni nguvu za Mungu tunazopewa ili tufanye bila kung’ang’ana mambo ambayo hatuwezi kufanya peke yetu. Mara tu tutakapong’amua ukweli kwamba kila kitu kizuri tulicho nacho hutujia kwa wema wa Mungu, ni kitu gani tunachobaki kufanya ila shukrani na kutoa shukrani?

Ni vigumu kumpa Mungu sifa tunapofikiria kwamba tunastahili kupata kile tunachopokea kutoka kwake. Lakini ni vigumu kukosa kumpa Mungu sifa tunapojua kwamba hatustahili kupata kile tunachopokea kutoka kwake—vyote ni kwa neema yake. Maisha yetu yanafaa tu kuwa mwitiko wa hayo yote.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwa neema yako. Bila neema yako kwa maisha yangu, nisingekuwa na tumaini. Lakini kwa sababu ya neema na nguvu zako, ninashukuru kwamba ninaweza kukamilisha mipango uliyo nayo juu ya maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon