Neema, Neema, Neema, na Neema Zaidi

Neema, Neema, Neema, na Neema Zaidi

…Na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi. WARUMI 5:20

Hatuwezi kuwa na shida ambayo ni kubwa sana kuliko neema ya Mungu. Shida zetu zikipata kuwa kubwa, shukuru kwamba neema ya Mungu inapata kuwa kubwa pia. Shida zetu zikizidi, ili twende kutoka moja hadi mbili, hadi tatu au zaidi, neema ya Mungu pia huzidi ili tuweze kukabiliana nazo.

Haijalishi vile shida zetu huenda zikawa, au zile tunazokabiliana nazo, tunaweza kutia imani yetu ndani ya Mungu ili kuzisuluhisha. Inachukua tu moyo wa shukrani, ulio na hakika kwamba Mungu ni mkubwa vya kutosha kushughulikia chochote kinachotukabili. Kisichowezekana kwa mwanadamu kinawezekana kwa Mungu.

Iwapo kuna kitu ambacho tunafaa kuwa tukifanya, Bwana atatupatia uwezo wa kukifanya. Hakuna vile atatuongoza katika hali bila kutuwezesha kufanya kile alichotuita kufanya. Chochote kile ambacho unakabiliana nacho leo, neema ya Mungu (nguvu ya kuwezesha) ni yako, na unaweza kufanya kinachohitajiwa kupitia kwa Kristo ambaye ni nguvu yako.


Sala ya Shukrani

Baba, ninapokabiliwa na shida nyingi mara moja, ninakushukuru kwa neema yako ambayo hunitosha. Ninashukuru kwa hakuna shida, au kiasi cha shida kilicho kigumu kwako.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon