Neema, nguvu ya Mungu ilyopeanwa bure

Neema, nguvu ya Mungu ilyopeanwa bure

Kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani. —Warumi 12:3

Ikiwa umeishi ulimwenguni humu kwa muda, utakubaliana name kwmba mara nyingi, mambo hayaendi jinsi ungetaka. Tunashukuru kwamba Mungu kamwe hataturuhusu katika hali yoyote ile bila kutupa uwezo wa kufurahi katika hali hiyo.

Ninaamini Mungu anatupa neema yake maalum kwa kila hali. Hivi ndivyo ninavyopenda kufafanua neema: “Nguvu ya Mungu kutusaidia kufanya chochote tunachohitaji kufanya.” Unaweza kuwa na nguvu  hiyo leo, lakini unapaswa kuipokea, na njia pekee ya kuipokea ni kwa imani.

Warumi 12: 3 inasema kwamba Mungu amemgawia  kila mtu kiasi cha imani

Jiulize leo, Ninafanya nini na imani yangu? Unaweka imani yako ndani yako mwenyewe, au kwa wengine, au kwa hali yako?

Hiyo sio kuishi katika neema, hiyo ni kuishi tu kwa nguvu zako mwenyewe na kazi zako. Na njia hiyo haiwezi kupata kazi kutendeka.

Lakini unapoachilia imani yako na kumtumaini Mungu kufanya kile ambacho huwezi kufanya, unaweka imani yako ndani yake

Kisha neema-nguvu za Mungu-zitakuja kupitia njia ya imani na itakuwezesha kufanya mambo ambayo yatakushangaza wewe na wengine.

Hapa ni ufafanuzi wangu wa neema tena: “Ni nguvu ya Mungu inayokuja kwetu bila malipo-maana haitugharimu chochote isipokuwa tu kuweka imani yetu kwa Mungu-kutuwezesha kufanya kwa urahisi kile ambacho hatuwezi kufanya kwa wenyewe na kiasi chochote ya mapambano au jitihada. ”

Weka imani yako kwa Mungu. Anataka kukupa neema Yake leo.


Ombi La Kuanza Siku

Mungu, najua kwamba maisha hayataenda kila namna nitakavyotaka, lakini ninakuamini. Kwa imani, napokea neema yako-nguvu uliyopewa kwa uhuru kunisaidia kutembea kupitia hali yoyote niliyo nayo leo

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon