Neema Yake Inatosha

Neema Yake Inatosha

Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamuwi chini ya sheria bali ya chini ya neema. —WARUMI 6:14

Neema ya Mungu ni kuu kuliko dhambi zetu au tatizo lolote ambalo tunaweza kuwa nalo. Huenda unahisi kuhukumika na kujaribiwa kuondoka katika uwepo wa Mungu, lakini anataka umkimbilie, sio kutoroka.

Sisi wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na ukamilifu wa Mungu, lakini Mungu ametoa suluhu kwa utata wetu kupitia kwa Yesu. Alituokoa kutokana na mateso yote ya dhambi na kutupatia neema yake ambayo hupokewa kiurahisi kwa imani.

Sisi sote tuna changamoto, mapambano na majaribu katika maisha, lakini Mungu wakati wote huwa yupo kutusaidia. Hakuna shida iliyo kubwa kumshinda. Huenda ukawa na kile kinaonekana kuwa mlima wa shida, lakini Mungu ana mlima wa neema ambao ni mkubwa zaidi. Hata kama hatustahili neema ya Bwana, bado ingalipo iwapo tutaomba kwa imani ya kawaida kama ya mtoto na kuamini!


Mungu huwa hatuongozi mahali ambapo hawezi kutukimu. Neema yake hututosha wakati wote—kwa kila hali zote za maisha.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon