. . . Na kupokea kwa upole Neno lile lililopandwa, liwezalo kuziokoa roho zenu. —YAKOBO 1:21
Kifaa cha nguvu kabisa na chenye mafanikio ya kuleta mabadiliko ya kweli na kudumu katika maisha yetu ni Neno la Mungu. Ni Neno la Mungu linalotuvuta na kutuleta karibu na Mungu.
Wakati wote shetani atajaribu kukudanganya, akikwambia vitu kukuhusu na kuhusu hali yako ambavyo ni kinyume na Neno la Mungu. Mradi tu tunaamini huo uongo, tutabaki tukiwa na dhiki, masikitiko na bila nguvu. Lakini Neno la Mungu la Ukweli likifunua uongo huo, ukweli unatuweka huru.
Ni Neno la Mungu pekee lililo na nguvu hizi, na ni Mungu pekee anayeweza kutubadilisha. Neno hufunua nia mbaya, mawazo mabaya, na maneno mabaya. Ukweli unaweza kutuweka huru kutokana na hukumu, kujikataa, lawama, kujichukia, kazi za mwili, na kila uongo ambao tumekubali na kuleta katika maisha yetu. Mungu anataka kutuweka huru ili tuweze kufurahia maisha ambayo ametupatia.
Upanga ulio katika ala hauna maana. Lazima utwaliwe na kutumiwa vizuri. Neno la Mungu ndilo upanga wa aaminiye, na tunaweza kujifunza kwa kuutumia kila siku, kulishusha ndani ya mioyo yetu, na kulinena katika kinywa chetu. Aaminiye anayefanya hivi amejaa nguvu na anaweza kuutimizia ufalme wa Mungu mambo makubwa.
Kusoma Neno ndiyo njia nambari moja ya kumkaribia Mungu.