Tena ipokeeni chapeo ya wokovu na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu. WAEFESO 6:17
Mungu hutupatia silaha za kushinda kila vita tunavyovikabili. Neno la Mungu ni upanga kwetu, na tunaweza kuutumia dhidi ya adui. Panga zetu haziwezi kutusaidia tukiziweka katika ala zao, jinsi tu vile Biblia haiwezi kutusaidia zikikaa kwenye rafu na kukusanya vumbi. Kutumia panga zetu ni kujua, kuamini na kusema Neno la Mungu.
Ukiamka asubuhi moja na uhisi unataka kukata tamaa, tumia upanga kwa kusema: “Sitakata tamaa! Ninashukuru kuwa Mungu ana mpango wa kunipa mustakabali na tumaini, na nitachuchumilia mbele kwa imani ili nishuhudie mipango hiyo” (tazama Yeremia 29:11). Mungu hutupa silaha za vita ili tuzitumie. Ukitaka kushinda, utaanza kujishughulisha. Utulivu na kutamani havishindi vita.
Sala ya Shukrani
Ninakushukuru, Baba, kwamba umenipa Neno lako na kwamba ninaweza kulitumia kushinda ushindi. Nisaidie kukumbuka kuegemea Neno lako badla ya nguvu zangu. Ninashukuru kwa ahadi zako zinazopitisha katika kila vita.