Ngao yako ya Imani

Ngao yako ya Imani

Zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mshale yote yenye moto ya yule mwovu. WAEFESO 6:16

Zamani askari jeshi walijikinga kwa ngao, na katika Waefeso 6:16, Biblia inasema kuhusu “ngao ya imani.” Kwa kuwa ngao hukinga, lazima imani ni njia ya kujikinga adui anaposhambulia. Tunaweza kushukuru kuwa Mungu hutupatia mfumo wa kujikinga. Lakini kama tu ilivyo na ngao ya kweli, ngao yake huweza kufanya kazi tu inapoinuliwa juu. Haitaweza kumsaidia askari jeshi kama imewekwa chini au kando yake.

Shetani anapotushambulia na hali ngumu au fikra zinazotufanya tushikwe na hofu, tunafaa kuinua ngao ya imani mara moja. Tunafanya hivyo kwa kuamua kwamba tutamwamini Mungu badala ya kujaribu kufikiria njia tutakazotumia kuishinda hali hiyo. Itasaidia kusema kwa sauti, ”Ninamwamini Mungu katika hali hii!” Sema kwa uthabiti ukiwa na imani. Yesu alimjibu shetani kwa kusema “Imeandikwa” akinukuu Andiko (tazama Luka 4), na tunaweza kufanya vivyo hivyo.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba Neno lako ni ngao ya nguvu, na linafanya kazi kinyume na kila kitu ambacho adui hujaribu kufanya katika maisha yangu. Imani yangu ina misingi yake katika Neno lako na ahadi zako juu ya maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon