Nguvu za Ajabu za Mungu

Nguvu za Ajabu za Mungu

Acheni mjue ya kuwa mimi ni Mungu, nitakuzwa katika mataifa nitakuzwa katika nchi! ZABURI 46:10

Tusipokuwa waangalifu, ni rahisi kutoona ukuu wa Mungu. Huwa tunaelekea kumfikiri, pamoja na uwezo wake kwa mtazamo wetu finyu. Lakini tusiwahi kusahau kwamba, Bwana anapoinuka, kila goti litapigwa na kila ulimi kukiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba (tazama wafilipi 2:10–11).

Tunamtumikia Mungu mkuu na aliye na nguvu, na tunaweza kushukuru kwamba ukuu wake unafanya kazi katika maisha yetu. Ninakuhimiza kutumia muda mwingi katika ibada na sifa, na muda mchache katika kupanga na kujaribu kumwambia Mungu anachohitaji kufanya. Mshukuru kwa wema wake na ukweli kwamba nguvu zake zinafanya kazi katika maisha yako..


Sala ya Shukrani

Baba, nisaidie kutambua vile ulivyo mwenye uwezo na nguvu. Asante kwamba hakuna adui anayeweza kukushinda na hakuna kinachoweza kukomesha kazi au mpango wako katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon