Nguvu za Kukabiliana na Mabadiliko

Nguvu za Kukabiliana na Mabadiliko

Jina la Bwana ni ngome imara; mwenye haki huikimbilia akawa salama. MITHALI 18:10

Watu wengi hawapendi mabadiliko. Aliyekuwa rais wa Marekani Wood- row Wilson alisema, “Ukitaka kutengeneza maadui, jaribu kubadilisha kitu.”

Mara nyingi tunapochoka au kuchoshwa tu na hali, tunakosa utulivu na kuanza kuomba: “Ee Mungu! Lazima kitu kibadilike!” Kisha Mungu anapojaribu kuleta mabadiliko katika maisha yetu, tunasema, “Bwana unafanya nini? Sidhani naweza kuvumilia mabadiliko haya!” Mara nyingi huwa tunajipata katika njia panda ya kutaka mabadiliko na kuogopa mabadiliko.

Shukuru Mungu kwamba huwa habadiliki. Kwa sababu yeye huwa yule yule, tunaweza kumwamini katika hali zozote zinazobadilika (tazama Waebrania 13:8, Malaki 3:6). Hili linafaa kutupatia himizo kuu na faraja tunapokabili mabadiliko katika maisha yetu. Hatuhitaji kuogopa mabadiliko; tunaweza kukabiliana nayo, kwa kuwa Mungu habadiliki.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba sina haja ya kuogopa mabadiliko. Hubadiliki na wewe ndiwe mnara wangu wa nguvu. Ninasimama kwenye msingi imara wa Neno lako na nitaishi kwa amani hata kama vitu vinabadilika kote karibu nami.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon