Mojawapo ya Vitu vya Nguvu ambavyo Unaweza Kufanya

Mojawapo ya Vitu vya Nguvu ambavyo Unaweza Kufanya

Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi. YOAHANA 13:35

Tukijisahau maksudi na kumfanyia mtu mwingine kitu—hata kama tunateseka—ni mojawapo ya vitu vya nguvu ambavyo tunaweza kufanya ili kushinda uovu. Shukuru kuwa Mungu anaweza kutusaidia kufanya hivyo.

Yesu alipokuwa msalabani akiteseka vikali, alichukua wakati kumfariji mwizi aliyekuwa karibu naye (tazama Luka 23:39–43). Stefano alipokuwa akipigwa kwa mawe, aliwaombea waliokuwa wakimpiga kwa mawe, huku akimuomba Mungu asiwahesabie dhambi hizo (tazama Matendo 7:59–60). Paulo na Sila walipokuwa gerezani, walichukua muda kumhubiria mlinzi wa gereza (tazama Matendo 16:27–34).

Iwapo tutapigana dhidi ya ubinafsi na tutembee katika upendo, ulimwengu utaanza kututambua. Hatutaufurahisha ulimwengu kwa kuwa tu kama wao. Lakini ni marafiki na jamaa wangapi ambao huenda wakaja kumjua Yesu kama tutawapenda kwa kweli badala ya kuwapuuza, kuwahukumu, au kuwakataa? Ninaamini ni wakati wa kutambua, nawe je?


Sala ya Shukrani

Baba, ninaomba kwamba utanipa uwezo wa kutanguliza mahitaji ya wengine kabla ya mahitaji yangu. Asante kuwa upendo wako una nguvu za kubadilisha maisha. Nisaidie kuonyesha nguvu hizo leo.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon