Ni Kitu Gani Kinakurudisha Nyuma?

Ni Kitu Gani Kinakurudisha Nyuma?

Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, …na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu… —WAEBRANIA 12:1

Mwandishi wa kitabu cha Waebrania alipoandika tuweke kando kila mzigo mzito, alikuwa anafikiria kuhusu wakimbiaji wa wakati huo ambao walikuwa wakivua nguo zao, na kubaki na nguo nyepesi ya kiunoni. Walihakikisha kwamba hakuna ambacho kingewazinga na kuwazuia kukimbia mbio kadri na uwezo wao. Walikuwa wanakimbia kushinda!

Sehemu muhimu ya kumkaribia Mungu ni kukagua maisha yetu na kuweka kando chochote kinachotuzinga au kutuondoa kwa Mungu. Kuwa katika uhusiano wa karibu naye hutuhitaji kuweka kando vitu vinavyomhuzunisha na kutuzuia, vitu vinavyotufanya tusiishi kulingana na mpango wake juu ya maisha yetu.

Mara nyingi tunahitaji kutazama maisha yetu na kuweka kando vitu vinavyotuzinga au kututoa kwa Mungu. Haiwezekani kukua kiroho bila kufanya hivyo. Mungu anapokuonyesha kitu cha kuweka kando, ninakuhimiza kufanya hivyo bila kusita. Usibishane na Mungu au kujisikitikia. Anachokuambia ufanye kitakufaidi mwishowe. Kama ni urafiki mbaya, tabia itakayodhuru, kukasirika, au hata dhambi kuwa jasiri ili ukabiliane nayo. Mwombe Mungu akusaidie halafu utoe nguvu kwake na kwa Neno lake.


Weka kando kila kitu kinachokuzuia na ukimbie mbio za utakatifu. Thawabu ni Mungu mwenyewe.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon