Lakini mimi nawaambia wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi. MATHAYO 5:44
Ni vigumu kuendelea kuonyesha upendo kwa wale watu ambao huchukua kutoka kwetu kila kitu tunachohiari kutoa na ambao hawatoi chochote. Lakini ninataka kukuhimiza kutokata tamaa. Hatuwajibikii tabia ya watu wengine, tunawajibikia yetu peke yake.
Ukweli ni kwamba Mungu hakukata tamaa juu yetu. Angefanyaje hiyvo? Yeye ni upendo, na upendo haukati tamaa—huwezi kushukuru kwa hilo? Upendo wakati wote huwa pale, ukifanya kazi yake. Upendo unajua ukikataa kukata tamaa, utakuwa na ushindi mwishowe.
Baadhi ya watu wanaweza kukataa kupokea upendo wetu hata tukifanya nini. Lakini hilo halimaanishi kwamba upendo umepungua. Upendo hututetea. Hutupatia furaha. Humpendeza Mungu tunapotembea katika upendo.
Sala ya Shukrani
Baba, ninapokabiliwa na mtu asiyeonekana kupokea upendo, hata hivyo nisaidie kuendelea kuwaonyesha upendo. Ninajua hakuna tendo lolote la upendo ambalo huharibika. Asante kwamba upendo haupungui.