Nia, Hiari, na Hisia

Maana ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe lakini sisi tunayo nia ya Kristo (1 WAKORINTHO 2:16)

Tunapomwalika Yesu kuja katika mioyo yetu, Roho Mtakatifu hufanya makao ndani yetu. Kutoka katika nafasi aliyo nayo mioyoni mwetu, ambayo pia ni kitovu cha utu wetu, Roho Mtakatifu huanza kazi ya utakaso katika nafsi zetu (nia, hiari na hisia).

Nia zetu hutuambia tunachofikiria sio kile ambacho Mungu anafikiria. Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yetu kubadilisha hilo. Lazima tujifunze kufikiria kwa kukubaliana na Mungu, jinsi ya kuwa vyombo vya Mungu anavyotumia kuwazia. Lazima fikra za kale zisafishwe na fikra mpya- kutoka kwa Mungu ziwe sehemu ya fikra zetu.

Hisia zetu hutuambia jinsi tunavyohisi, sio vile Mungu anavyohisi kuhusu hali, watu, na uamuzi tunaofanya. Kulingana na Zaburi 7:9, Mungu hupima na kujaribu hisia. Hufanya kazi nasi hadi tunapoacha kuathiriwa na hisia za kibinadamu ila tu kuathiriwa kwa Roho.

Hiari zetu hutuambia tunachotaka, sio anachotaka Mungu. Hiari huenda kinyume na hisia na hata fikra. Tunaweza kuitumia kufanya kitu kilicho sawa hata kama hatujihisi kukifanya. Tuna hiari huru, na Mungu hawezi kutulazimisha kufanya chochote. Anatuongoza kwa Roho wake katika kile anachojua kitakuwa kizuri kwetu, lakini uamuzi wa mwisho huwa juu yetu kuufanya. Mungu hutaka tufanye uamuzi ambao kila mara unakubaliana na mapenzi yake, sio yetu.

Kadri haya maeneo matatu- nia, hiari na hisia yanavyokuja chini ya utawala wa Yesu Kristo na uongozi wa Roho Mtakatifu, tutazidi kukomaa kama waaminio.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Unaweza kudhibiti hisia zako badala ya kuziacha zikudhibiti.  

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon