Nia ya Utiifu

Nia ya Utiifu

Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, masikio yangu umeyazibua, kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka. ZABURI 40:6

Mungu hupendezwa na utiifu wetu. Anataka kutuongoza na kutuelekeza, lakini haisaidii iwapo hatuko tayari kusikiza na kutii. Ametupatia uwezo wa kumsikiza na kumtii. Mungu hahitaji dhabihu kubwa kuliko utiifu wa moyoni.

Baadhi ya mambo ambayo Mungu atakuambia ufanye yatakuwa ya kusisimua, na mengine hayatasisimua, lakini kwa vyovyote vile, tunafaa kuwa tayari kumfuata. Tunaweza kushukuru tukijua kwamba anachotuambia tufanye kitaishia kuwa chema iwapo tu tutakifanya kwa njia yake.

Ukitaka mapenzi ya Mungu kwa ajili ya maisha yako, ninaweza kukwambia resipe hiyo kwa njia rahisi sana: Ommba ana utii. Mungu amekupa uwezo wa kufanya yote mawili.


Sala ya Shukrani

Baba, ninashukuru kwamba unasema na moyo wangu na kunielekeza katika njia inayofaa. Licha ya vile inavyoonekana kwamba mambo ni magumu, ninataka kutii sauti yako na kuamini kwamba mpango wako juu ya maisha yangu ni mzuri kabisa. Asante kwa kunipenda na kunena na moyo wangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon