Njia iliyo Bora Kabisa

Takeni sana karama zilizo kuu. Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora  (1 Wakorintho 12:31)

Wakorintho wa kwanza 13, ambayo inafuata mara moja andiko la leo inatuambia wazi kwamba haijalishi idadi ya karama za Roho Mtakatifu zinazofanya kazi ndani yetu iwapo hatutazitumia kwa upendo tutakuwa tunafanya kazi bure. Kulingana na andiko la leo, upendo ni njia bora zaidi na ni bora kuliko vitu vingine vyote.

Tukiomba katika ndimi za watu na malaika, na tuwe na uwezo wa kinabii, tuweze kuelewa siri, na hata kuwa na maarifa yote na imani inayoweza kuhamisha milima, lakini tusiwe na upendo, sisi “si kitu” (soma 1Wakorintho 13:2).

Katika siku za awali za kujazwa na Roho katika safari yangu na Mungu nilisikia mazungumzo mengi kuhusu karama za Roho. Watu wengi walizingatia karama walizokuwa nazo na vile walivyoweza kuzitumia. La kuhuzunisha ni kwamba nilisikia mengi kuhusu karama za kiroho kuliko nilivyosikia kuhusu upendo au tunda linginelo la Roho.

Kuna karama tisa za Roho zilizoorodheshwa katika 1 Wakorintho 12 na nyingine nyingi katika Warumi 12. Kuna matunda tisa ya Roho yaliyoorodheshwa katika Wagalatia 5. Karama za Roho ni muhimu sana na, tunafaa kuzitamani.

Tunahitaji kujifunza kuzihusu, kujua jinsi ya kuzitumikisha inavyofaa, na kuhakikisha unakuza karama uliyopewa. Lakini hatufai kutilia mkazo karama au uwezo wa kutumikisha karama hizo kuliko tunavyosisitiza kutumika katika upendo.

NENO LA MUNGU KWAKO LEO:

Mungu anakupenda na anataka upendo wake utiririke kutoka kwako hadi kwa wengine.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon