Njia Nzuri Zaidi Ya Kuanza Maombi

Njia Nzuri Zaidi Ya Kuanza Maombi

Nao wasimame kila asubuhi kumshukuru na kumsifu Bwana, na jioni vivyo hivyo. 1 MAMBO YA NYAKATI 23:30

Hata tuwe tunaomba kwa ajili ya jambo gani, tunaweza kushukuru wakati wote tunapoomba. Desturi nzuri ya kuanzisha ni kuanza maombi yetu yote kwa shukrani. Mfano wa hilo utakuwa: “Asante, Baba, kwa yote ambayo umetenda maishani mwangu; Wewe ni wa kuheshimiwa na kwa kweli nakupenda na kukushukuru.”

Ninakuhimiza kuchunguza maisha yako, kuzisikiza fikra zako na mawazo yako, na kuona kiasi cha shukrani unazotoa, Unanung’unika na kulalamika kuhusu mambo au umejawa shukrani?

Ukitaka kujaribu hili, hebu jaribu kukaa siku nzima bila kutamka neno lolote la lalama. Anza kuwa na moyo wa kushukuru katika kila hali. Kwa kweli kuwa tu mwenye shukrani kijeuri—na utazame vile undani wako na Mungu utakavyoongezeka anapomwaga baraka zaidi kuliko alivyofanya awali.


Sala ya Shukrani

Asante, Baba, kwa vile unavyoniongoza katika maombi. Nisaidie kuja kwako kwa shukrani kabla sijafanya jambo lolote. Acha shukrani ziwe msingi wa maisha yangu ya maombi. Leo ninaamua kuweka malalamiko kando na kuwa mwenye shukrani katika maombi badala yake.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon