Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, wasije wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na vita, na kurudi Misri. —Kutoka 13:17
Mungu aliwaongoza wana Israeli katika njia ndefu ngumu ndani ya jangwa kwa sababu alijua hawakuwa tayari kwa vita ambavyo wangekabiliana navyo ili kumiliki Nchi ya Ahadi. Alihitaji kufanya kazi ndani ya maisha yao kwanza, kuwafundisha Yeye alikuwa nani na kwamba wasingejitegemea.
Unaweza kuhakikishiwa kwamba popote Mungu anakuongoza anaweza kukulinda. Huwa haruhusu mambo mengi kuja kinyume chetu kuliko tuwezavyo. Si lazima tuishi kwa kung’ang’ana kila wakati iwapo tutajifunza kumwegemea mfululizo kwa ajili ya nguvu tunazohitaji.
Ikiwa unajua Mungu amekwambia ufanye kitu, usijiuzulu kwa kuwa kimekuwa kigumu. Mambo yanapokuwa magumu, tumia muda mwingi zaidi naye, mwegemee zaidi, na upokee neema zaidi kutoka kwake (Waebrania 4:16) Neema ni uwezo wa Mungu unaokujia bila malipo yoyote, ili kufanya kupitia kwako usiyoweza kufanya mwenyewe.
Mungu anajua kwamba njia rahisi, mara nyingi huwa sio nzuri sana kwetu. Ndiyo kwa sababu ni muhimu kutokata tamaa, kuchoka na kuzimia.
Shetani anajua kuwa akiweza kutushinda katika fikra zetu, anaweza kutushinda katika tajriba yetu.