Njia ya Mungu Huwa na Nafuu Wakati Wote

Njia ya Mungu Huwa na Nafuu Wakati Wote

Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini. ISAYA 26:3

Huenda vitu visiende vile tunavyotaka kila wakati maishani, lakini tunaweza kuamini kwamba njia ya Mungu ni afadhali. Mungu ni Mungu mwema, na alisema kuwa ana vitu vizuri ambavyo amewapangia wanawe: “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho” (Yeremia 29:11).

Hatuhitaji kuogopa mabaya, kwa sababu Mungu sio hakimu aliye na hasira; sio mchoyo. Ni mwema. Tunaweza kufurahia, kwa shukrani, tukijua kwamba kila kitu kizuri katika maisha hutoka kwa Mungu. Anataka tumwamini, na tunapochukua hatua ya imani kufanya hivyo, tutaona wema wa Mungu ukidhihirika katika maisha yetu. Kadri tunavyojisalimisha, ndivyo maisha yanakuwa nafuu.


Sala ya Shukrani

Baba, nikijipata nimesikitishwa na hali zangu, nisaidie kukumbuka kwamba uko mamlakani. Ninakushukuru kwamba mpango wako juu ya maisha yangu ni mwema sana kuliko mpango wangu mwenyewe. Ninakuamini pamoja na uongozi wako katika maisha yangu.

Facebook icon Twitter icon Instagram icon Pinterest icon Google+ icon YouTube icon LinkedIn icon Contact icon